Mkufunzi mkuu wa klabu ya Newcastle United mwite Eddie Howe amesema madai ya kwamba sajili mpya ya Al Nasr Christiano Ronaldo ameweka kipendele cha kurudi uingereza na kuchezea Newcastle iwapo itafuzu kuingia mashindano ya Uefa Champions league msimu ujao ni porojo tupu na hayana ukweli wowote.
Ronaldo alitambulishwa rasmi jana kwa mashabiki wa Al Nassr baada ya kuhamia Saudia Arabia kwa uhamisho uliogharimu Euro milioni 200.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 37 ambaye pia ni mshindi mara tano wa Ballon Dor aliachana na Manchster united baada ya kugongana na uongozi wa klabu hiyo pamoja na mahojiano ya kukashifu Uongozi wa Manchester United jambo ambalo lilipelekea mkataba wake kukatishwa rasmi mwezi disemba kabla ya mashindano ya dunia nchini Qatar.

