Uongozi wa soka la mashinani kwenye eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi umewaonya vilali vilabu vilivyosajiliwa na shirikisho la tawi hilo kutotumia wachezaji kutoka maeneo bunge mengine na wanaochezea ligi tofauti katika mashindano yoyote yanayosimamiwa na shirikisho la fkf Magarini.
Katika waraka uliochapishwa mitandaoni na katibu wa soka Emmanuel Kazungu umeibua madai kwamba klabu ya Bosuster fc pamoja na Uhuru super stars wamekuwa wakitumia wachezaji wa eneo bunge la malindi wakitokea vilabu vinavyoshiriki ligi za mkoa. Daraja la pili lakini pia daraja la kwanza kitaifa.
Kwa sasa uchunguzi wa madai hayo unaendelea na huenda vilabu hivyo vikaadhibiwa vilivyo na kuongeza kwamba iwapo vilabu vingine vitashuhudiwa kushiriki katika ulaghai huo vitaondolewa ushindi wao wote pamoja kubanduliwa kabisa katika mashindano.

