Rais William Samoei Ruto amesema gharama ya juu ya umeme nchini itashughulikiwa baada ya wadau husika kufanya utathmini upya wa bei ya kawi kulingana na muda ambao umetengwa kisheria.
Akizungumza jana akiwa kwenye ikulu ya Nairobi katika mahojiano na wanahabri, Rais Ruto amesema kwa sasa serikali inaendeleza mikakati kuhakikisha gharama ya umeme inapungua nchini ili kuwanusuru wakenya dhidi kugharamika zaidi.
Wakati huohuo akizungumzia suala la gharama ya juu ya maisha kwa wananchi, Rais Ruto amesema wanaendeleza mipango ya kilimo cha ekari elfu 10 katika mradi wa Galana Kulalu kuanzia mwezi ujao wa Februari mwaka huu wa 2023.
Aidha, akizungumzia uagizaji wa chakula cha GMO, Rai Ruto amesema wanasayansi nchini wamethibitisha kuwa chakula hicho ni salama na kwa muda sasa serikali imekuwa ikiagiza chakula chenye kiwango cha GMO.
RAIS RUTO AELEZA MATUMAINI YA KUPUNGUA KWA GHARAMA YA UMEME NCHINI

