Waziri wa usalama wa ndani Prof. Kithure Kindiki ametangaza kubadili mfumo wa oparesheni ya kukabili wahalifu katika kaunti ya Lamu.
Kindiki aliyezuru eneo hilo jana ambalo lililoshuhudia mashambulizi kadhaa majuma yaliyopita ameamuru kuajiriwa kwa askari 100 wa akiba NPR watakaokabidhiwa bunduki kudumisha usalama.
Ujio wa Kindiki katika kaunti hiyo unajiri baada ya mashambulizi kadhaa yaliyosababisha vifo vya jumla ya watu wanne chini ya Mwezi mmoja.
Amesema mikakati ambayo wameweka itasaidia katika kuwakabiliwa wahalifu ambao wamekuwa wakiwahangaisha wenyeji.
Aidha, amewapongeza askari wa NPR kwa kuwakabili wahalifu ambao walivamia eneo la Ziwa la Taa siku ya Krismasi mwaka jana 2022 na kuahidi kuongeza askari hao wa akiba katika maeneo yote ya Kaunti ya Lamu ambayo yanashuhudia ukosefu wa usalama.
Ni kauli ambayo imeungwa mkono na baadhi ya viongozi akiwemo gavana wa kaunti ya Lamu Issa Abdalla Timamy na mbunge wa Lamu Magharibi Stanley Muthama ambao wamehimiza umuhimu wa ushirikiano baina ya asasi za usalama na wenyeji ili kuimarisha usalama kwenye kaunti ya Lamu.
Suala la umiliki wa ardhi limetajwa kuwa chanzo cha visa hivyo kushuhudiwa katika kaunti ya Lamu.
Kufikia sasa watu wanne wamepoiteza maisha yao ikiwa ni pamoja na maafisa wa KDF wanaoendeleza oparesheni dhidi ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la Al – Shabaab hasa kwenye msitu wa Boni.
ASKARI 100 WA NPR KUONGEZWA KAUNTI YA LAMU

