Batoto ba mungu Sofapaka ndio mabingwa wa kombe la Jamhuri baada ya mechi ya jana katika uwanja wa Nyayo ambapo vijana hao waliwatandika AFC Leopards kupitia ufundi wa upigaji wa matuta.
Katika dakika ya 14 ya mchezo Washington Munene aliwatanguliza Ingwe kabla Roddy Manga kusawazisha bao hilo kunako dakika ya 84 ya mchezo baada ya Jaffary Owitti kufanyiwa madhambi katika kisanduku cha goli.
Mechi hiyo pia inatambulika na FKF kama mechi ya ligi kuu kwani matokeo ya mechi hiyo yanasalia kuwa sare ila ililazimika kwenda matuta ili kubaini bingwa wa kombe la Jamhuri hapo jana.

