MESSI KUSTAFU SOKA LA KITAIFA BAADA YA FAINALI ZA MWAKA HUU.

Lionel Messi mchezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona ambaye kwa sasa anakipiga kunako klabu ya Paris SG amethibitisha kwamba atakuwa anastafu rasmi soka la kimataifa baada ya kucheza fainali za siku ya jumapili wakati ambapo mashindano ya kombe la dunia yatakuwa yanatamatika rasmi.

Hii itakuwa ni mara ya pili Messi atakuwa anacheza fainali za kombe la dunia baada ya mwaka 2014 ambapo Argentina ilipoteza kwa Ujerumani kwa bao moja bila jawabu goli ambalo lilifungwa na Mario Gotze katika dakika za lala salama.

Kufikia sasa messi anaongoza kwa ufungaji wa mabao katika mashindano ya kombe la dunia akiwa ameingia kamabani mara tano na kutoa asisti tatu.

Mechi ya mwisho anayotarajia kucheza mshindi huyo mara saba wa Ballon Dor itakuwa siku ya Jumapili ambapo Argentina watakuwa wanavaana na Ufaransa katika fainali za kombe la dunia.