SOKA LA RABAI KUIMARISHWA NA MIKATABA YA WACHEZAJI – JOHN BARISA

Shirikisho la soka tawi la eneo bunge la Rabai kaunti ya Kilifi linalenga kuanzisha utaratibu wa mikataba rasmi kwa wachezaji pamoja na vilabu ili kukabili tatizo la wachezaji kutofuata sheria wakati wa uhamisho.

Akizunguimza na Tama la Spoti John Barisa ambaye ni katibu mkuu wa shirikisho hilo amesema kwamba mwakani wanamalengo ya kuanza kuwasilisha mikataba rasmi kwa wachezaji, mazungumzo na maridhiano kufanyika kabla mchezaji kufanya uhamisho rasmi, jambo ambalo ametaja kuwa litaonyesha makuzi ya soka la mashinani lakini pia taaluma kwa ujumla.

Hata hivyo ameshauri wanasiasa kupiga jeki michezo ya mashinani katika nyakati zote sio kipindi cha kampeni pekee ikizingatiwa kwamba wachezaji mashinani wanapitia changamoto nyingi ambazo anahofia huenda zikalemaza michezo iwapo wachezaji watakosa kusaidika