HATUTAPELEKA WABUNGE QATAR, ASEMA KARANI WA BUNGE LA KITAIFA

Karani wa bunge la kitaifa Samuel Njoroge amekanusha madai kwamba bunge la kitaifa linalenga kutuma wabunge kwa ziara ya kombe la dunia nchini Qatar mashindano ambayo yanaanza rasmi siku ya Jumapili.

Njoroge anasema mpaka kufikia sasa hajapokea pendekezo lolote kutoka mhasibu wa bunge hilo na kusistiza kwamba bunge la kitaifa kwa sasa linatilia mkazo kusitisha matumizi yasokuwa ya lazima ya pesa za mlipa ushuru.

Haya yanajiri baada ya taarifa za awali kutoka kwa baadi ya wabunge kwamba wanalenga kutuma wabunge 15 nchini Qatar kwa ziara ya kombe la dunia.

Ikumbukwe kwamba mwaka wa 2018 bunge hilo lilituma maafisa 25 kutoka bunge hilo kwenda urusi kwa ziara ya kombe la dunia jambo ambalo lilikashifiwa na wakenya ikizingatiwa kwamba wabunge hao walikosa kuandika ripoti nzuri ya ziara hiyo na kutajwa kama njia ya kufuja hela za umma.

Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi amekiri hadharani kwamba ni kati ya wanaziara watakaoandamana na spika wa bunge la kitaifa Moses Masika Wetangula.