YAPENI MASHINDANO YA DUNIA HESHIMA YAKE – GIANNI INFANTINO

Raisi wa fifa Gianni Infantino ameomba kusitishwa kwa mapigano yanayoendelea Ukraine kwa muda wa mwezi mmoja kwa heshima ya mashindano ya kombe la dunia ambayo yatakuwa yanaendelea kwa kipindi cha siku 28.

Infantino anasema ni muda sasa mataifa yanafaa kuja pamoja na mapigano ya urusi na Ukraine yanachoma picha ya mashindano ya kombe la dunia ambayo kati ya malengo yake ni kuleta watu pamoja na kuachana na tofauti zao.

Amesema sasa ni wakati wa mataifa hayo yanayozozana kuja pamoja na kuanza mazungumzo ya amani na kuondoa uhasama walonao ambao umeleta uharibifu mkubwa pamoja na vifo vya mamluki wengi.