Wawakilishi wadi wa kaunti ya kilifi wamebuni mbinu ambazo zitasaidia kaunti hii kukuza talanta na michezo, tamaduni miongoni mwa vijana.
Wakiongozwa na makamu mwenye kiti wa jinsia utamaduni na sana na michezo katika bunge hilo Maurice wanje ambaye pia ni mwakilishi wadi ya ganda viongozi hao wamesema tayari wamebuni hoja zitakazowasilishwa katika bunge hilo ili kuwezesha serikali ya kaunti hiyo kujenga viwanja vidogo vya michezo katika maeneo bunge saba, na uwanja mkuu wa michezo pamoja na mikutano cha kaunti.
Kwa upande wake Rashid Odhiambo ambaye ni mwakilifi wadi wa Malindi town ward anasema kwamba iwapo viongozi watashirikiana katika kuekeza kwenye muondo mbinu ya talanta, vijana wanaweza kujiajiri kupitia talanta hizo na kuepuka kujiingiza katika mambo potovu ikiwepo matumizi ya dwa za kulevya.

