Idara ya afya kaunti ya Kilifi inaendeleza shughuli za kuwarai wananchi kutoa damu itakayosaidia kuwahudumia baadhi ya wagonjwa, katika hospitali ya rufaa ya kaunti hapa mjini Malindi na maeneo mengine ya kaunti ya Kilifi
Kwa mujibu wa afisa mkuu anayehusika na masuala ya ukusanyaji wa damu katika kaunti hii Lazima Katana, ongezekya Kilifi.
Akizungumza na lulu fm amesema wanalenga kukusanya takriban panti mia mbili kumi na tano za damu, katika eneo la seven to seven mjini Malindi.
Aidha, amesema kuwa zoezi hilo hufanyika kila baada ya miezi minne katika maeneo mbalimbali ya kaunti hii na kuongeza kuwa ipo haja ya watu wengi zaidi kujitokeza na kusaidia kunusuru maisha ya wagonjwa walioko katika vituo vya afya kaunti hii kupitia hatua ya wao kushiriki zoezi hilo la kutoa damu.