Mbunge wa Matuga kaunti ya Kwale Kassim Sawa Tandaza ameitaka idara ya usalama kaunti ya Kwale kukabiliana na magenge ya kihalifu yanayowahangaisha wakaazi wa eneo hilo.
Tandaza amesema kuwa siku za hivi karibuni kumekuwa na visa vingi vya uhalifu vinavyotekelezwa na vijana kwenye maeneo mbalimbali ya eneo bunge hilo.
Mbunge huyo ametoa wito kwa wazazi kutowatetea wanao wanaojihusisha na utovu wa usalama kwani wao ndio chanzo cha visa hivyo kukosa kudhibitiwa.
Tandaza amesema kuwa kwa sasa anapania ya kuimarisha usalama katika eneo bunge hilo kwa kudumisha vituo vya polisi kwenye maeneo kadhaa ya Matuga.
KASSIS SAWA TANDAZA ALALAMILIA UTOVU WA USALAMA KATIKA ENEO BUNGE LAKE

