Serikali ya kaunti ya Lamu imewahikikishia usalama wa kutosha wageni pamoja na wenyeji wanaotarajiwa kuhudhuria sherehe za kitamaduni zinazotarajiwa kufanyika mwezi huu.
Kamishna wa kaunti ya Lamu Irungu Macharia amesema kuwa maafisa wa usalama kwenye vitengo vyote wameagizwa kushika doria kudumisha usalama ikiwa zimesalia wiki mbili pekee kabla ya kufanyika kwa sherehe hizo kisiwani amu.
Zaidi ya wageni elfu 30 wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hizo miongoni mwao wakiwa mabalozi huku naibu rais Rigathi Gachagua akiwa mgeni mheshimiwa ambaye atafungua rasmi sherehe hizo.
Vijana na wakaazi kwa jumla katika kaunti hiyo ya Lamu watanufaika pakubwa kiuchumi kutokana na sherehe hizo kwani kutakuwa na shughuli nyingi za kibiashara.
Ali Abbas ni mwanakamati wa kamati inayoandaa sherehe hizo za kitamaduni.
