KENYA SHUJAA YAINGIA KATIKA RATIBA YA MASHINDANO YA DUNIA

Timu ya taifa ya kenya ya raga kikosi cha wachezaji saba kila upande waite Kenya Shujaa wamepangwa katika Kundi D pamoja na timu ya taifa ya Argentina, Ireland na Kanada katika msururu wa ufunguzi wa raga ya wachezaji saba duniani kwa msimu wa 2022/2023 huko Hong Kong mwezi Novemba 4 hadi 6.
Kenya Shujaa walimaliza katika nafasi ya 12 msimu uliopita wakiwa na alama 49, na watakuwa wakitafuta kuboresha kiwango chao baada ya kumaliza nafasi ya 6 kwenye mkondo wa mwisho ya Los Angeles, nafasi ambayo ilikuwa yao ya juu zaidi katika muhula huo.

Mabingwa Australia wako kwenye kundi A pamoja na New Zealand, Samoa na wenyeji Hong Kong huku Afrika Kusini wakiwa katika Kundi B pamoja na Ufaransa, Uingereza na Uruguay.