BAA LA NJAA LAZIDI KUWAATHIRI WANAFUNZI KAUNTI YA KWALE

Afisa wa idara ya watoto katika kaunti ya Kwale Zephaniah Apoko ametoa wito kwa wizara ya elimu kuhakikisha shule za umma kwenye kaunti hiyo zinaboresha mpango wa lishe kwa watoto shuleni.
Apoko ameutaja mpango huo kuwa wenye manufaa kwani utasaidia wanafunzi kusalia shuleni bila kusitisha masomo yao kutokana na baa la njaa ambalo linaendelea kukabili baadhi ya maeneo nchini.
Amesema wanafunzi wengi wamekuwa wakisitisha masomo yao kutokana na hali hiyo na ni vyema iwapo hilo litatiliwa maanani.