Rais wa shirikisho la soka fkf Nick Mwendwa analenga kutangaza tarehe za kuanza arasmi kwa msimu mpya wiki hii, msimu ambao alikuwa amedokeza awali kwamba utaanza mwishoni mwa mwezi huu.
Aliyasema hayo katika ujumbe alioachapisha kwenye mtandao wake wa twitter na kuongeza kwa kuwashauri wachezaji, makocha pamoja na washikadau wengine kuzidisha mazoezi wanaposubiri tarehe rasmi ya kuanza kwa msimu wa fkf wa 2022/2023.
Wakati hayo yakijiri wakufunzi hapa nchini akiwemo naibu mkufunzi katika klabu ya AFC Leopards mwite Tom Juma amesema kwamba sontofahamu ya tarehe rasmi kunawafanya wachezaji kukosa morali wa kupiga tizi akisema kuwa wanakosa uvumilivu wa suuubra nyingi ambazo mbivu zake zinakawia kuiva.

