Ipo haja ya baadhi ya mila na tamaduni zinazokandamiza maisha ya mtoto wa kike katika jamii kutupiliwa mbali.
Haya ni kwa mujibu wa rais wa bunge la vijana kaunti ya Kilifi Jacinta Mbeyu Sanga, ambaye amesema baadhi ya watoto wa kike wamekosa kupata nafasi za kuboresha maisha yao, hasa katika masuala ya uongozi kutokana na mila na tamaduni, zinazopinga uongozi wa wanawake katika jamii mbalimbali Afrika.
Akizungumza na mwanahabari wetu kwa njia ya simu, Mbeyu amesema wanawake wengi hupigwa vita katika uongozi wao jambo ambalo, huchangia hatua ya wao kukosa kufanikisha maono yao.
Wakati huohuo amesema jinsia ya kike imeendelea kudhulumiwa hasa katika masuala ya kupata ajira, kwa madai kuwa wengi hulazimishwa kufanya ngono ili kupewa ajira jambo ambalo, amesema linapaswa kuangaziwa na wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
.
JACINTA MBEYU ASEMA KUNA HAJA YA MILA NA TAMADUNI ZINAZOKANDAMIZA MTOTO WA KIKE KUTUPILIWA MBALI

