MERAB SHIBUYANGA AWAHIMIZA WAZAZI KAUNTI YA KILIFI KUWA KARIBU NA WATOTO WAO

Mwenyekiti wa masuala ya amani katika shirika la County Women Peace and Security kaunti ya Kilifi, Merab Shibuyanga amewahimiza wazazi kuhakikisha wanazungumza na watoto wao, kuhusiana na masuala ya ngono.
Akizungumza na meza yetu ya habari, amesema wazazi wengi wangali wanafuata mila na tamaduni hali ambayo, inawafanya kutokuwa huru kuzungumzia suala hilo ili kuwaepusha na visa vya mimba za utotoni.
Amesena iwapo wazazi watachukua jukumu hilo la kuwa karibu na watoto wao na kuzungumza nao kuhusu athari za kufanya ngono wakiwa na umri mdogo basi huenda wakakabiliana na tatizo la mimba za utotoni.
Aidha, ametoa wito kwa wazazi kutenga muda wa kukaa na watoto ili kuwa na uhusiano thabiti nao na pia kujua changamoto zinazowakumba.