Mkufunzi mkuu wa kikosi cha kinadada wa malkia strikers Paul Bitok amempongeza Sharon Chepchumba mchezaji wa volibali kwa kusaini dili kubwa na klabu ya Aris Thesaloniki ya Ugiriki kwa mkataba wa uhamisho wa kudumu.
Chepchumba ambaye alianza kucheza kama kipa wa soka kabla ya kuhamia kwenye mchezo wa mpira wa wavu sasa amesaini mkataba wa miezi sita na klabu Aris Thesaloniki huku Paul Bitok akikiri kwamba Sharon amekuwa na safari ndefu iliyojaa kujituma tangia akiwa shule ya upili ya Kwanthanze ambao msimu huu waliingia katika fainali za shule za upili afrika mashariki mashindano yaliyofanyika mjini Arusha Tanzania.
Paul Bitok aidha amepongeza klabu ya KCB aliyokuwa anachezea Sharon kwa kumwachia akisema anajivunia kumwona mchezaji huyo akicheza kimataifa, ikizingatiwa kwamba Paul Bitok mwenye ashawahi kuhudumu kama mchezaji wa kulipwa akiwa nchini Croatia.

