Serikali ya kaunti ya Kilifi imeombwa kuwaweka kwenye mpango wa malipo wakunga wa vijijini wanaotoa huduma muhimu kwa wanawake wajawazito mashinani.
Kwa mujibu na Philomena John ambaye ni mkunga kutoka eneo bunge la Magarini kaunti ya kilifi, maeneo yaliyo mbali na hospitali wanawake wamekuwa wakitegemea huduma za haraka kutoka kwa wakunga.
Philomena amesema hatua hiyo itawachachawiza wakunga hao wa mashinani kutekeleza jukumu lao vyema zaidi ikizingatiwa wamekuwa wa msaada kwa kina mama wajawazito ambao hushindwa kufika kwenye vituo vya afya.
Amesema changamoto kuu inawakumba wakunga wa mashinani ni ukosefu wa vifaa vya kutosha vya kuwahudumia kina mama wengi wajawazito hasa wale wanaohitaji kuongezwa damu na maji mwilini.
SERIKALI YA KAUNTI YA KILIFI YAOMBWA KUWAWEKA KWENYE MPANGO WA MALIPO WAKUNGA WA VIJININI

