UKATAJI WA MITI KIHOLELA INACHANGIA KUHARIBU MAZINGIRA KANDA YA PWANI

Ukataji miti kwa minajili ya kutengeneza makaa ili kujikimu kimaisha umetajwa kuchangia uharibifu wa mazingira ukanda huu wa pwani.
Haya ni kwa mujibu wa mwakilishi wa vijana katika baraza la wazee wa kaya ukanda wa pwani, Nguma Charo Kenga ambaye amesema ukataji huo wa miti unaharibu mazingira.
Kenga amesema huenda vijana wengi wakakosa kukimu mahitaji yao ya kimsingi, iwapo watasitisha suala la ukataji wa miti kwani ukosefu wa ajira umewapelekea kuingilia uchomaji wa makaa.
Akizungumza na vijana Nguma amesema kuwa ipo haja ya viongozi waliochaguliwa katika ngazi mbali mbali kaunti hii, kujitokeza na kutatua suala la ukosefu wa ajiria kwa jamii.
Ameongeza kuwa baadhi ya vijana wamekuwa wakielekea katika mataifa ya uarabuni ili kutafuta ajira licha ya eneo hili kuwa na rasilimali nyingi ambazo, huenda zikawasaidia wananchi katika kupata kipato kitakachowasaidia kukimu mahitaji yao muhimu huku akitoa wito kwa viongozi, kuweka kando tofauti zao za kisiasa na badala yake kuungana ili kutatua matatizo yaw a Pwani.