VILABU VYA KPL VYAOMBA UHAKIKA WA MWANZO WA MSIMU MPYA

Mkufunzi wa klabu ya AFC Leopards Patrick Aussems ameomba uongozi wa soka kutoa thibitisho tosha la iwapo msimu mpya wa mwaka 2022/2023 utaanza lini kwani mpaka sasa vilabu vingi viko gizani kuhusiana na mstakabali wa soka nchini Kenya.

Amekuwa akiyasema hayo wakati ambapo shirikisho la soka nchini Kenya linasalia kuwa haramu baada ya kuvunjwa na waziri wa michezo balozi amina Mohamed na licha ya Nick Mwendwa kusema kwamba sasa amerejea kwenye wadhifa wake huku kamati ya mpito iliyoteuliwa kusimamia soka muda wake ukielekea kutamatika.

Awali kulikuwa na taarifa kutoka kwa kamati ya mpito kuwa msimu ungeanza tarehe 24 mwezi huu huku Mwendwa ambaye baada ya kuapishwa kwa rais mpya wa taifa la Kenya dkt William ruto akisema kwamba msimu mpya utaanza rasmi mwezi ujao tofauti na tarehe iliyotoliwa na kamati.

Mkurufunzi Patrick anasema vijana wake wanazidi kupiga msasa mchezo wao baada ya kupiga sare mbili kwenye mechi za kirafiki dhidi ya talanta lakini pia ulinzi stars huku akiwa na iamni kwamba watafanya vyema msimu ujao tofauti na msimu uliotamatika waliomaliza katika nafasi ya tano.