Mratibu wa kitaifa wa idara ya maendeleo ya miji na nyumba Peris Mangira amethibitisha kuwa zaidi ya hati miliki 700 zimekabidhiwa wenyeji wa Kaunti ya Kilifi kupitia mradi wa serikali wa kubadilisha maisha na makazi ya mitaa ya mabanda almaarufu KISIP.
Peris Mangira amesema wamefanikiwa kutoa stakabadhi hati miliki 900 katika awamu ya kwanza huku familia zaidi zikitarajiwa kunufaika na katika mpango huo ambao unafadhiliwa na benki ya Dunia na kutekelezwa na serikali ya kitaifa kwa ushirikiano na serikali za kaunti.
Vilevile amesema mikakati zaidi imewekwa kuhakikisha hilo linafanikishwa ipasavyo na Kaunti ya Kilifi ni miongoni mwa kaunti zingine 33 zilio na Mitaa ya mabanda itakayoboreswa kupitia mpango huo.
Kwa upande wake Gavana wa Kaunti ya Kilifi Gideon Mungaro amesema mpango huo unalenga mitaa mbalimbali kama ya Kibokoni, Kibaoni na Shingila miongoni mwa mingine ambayo imekuwa katika hali mbaya.
ZAIDI YA HATI MILIKI 700 ZAKABIDHIWA WENYEJI WA KAUNTI YA KILIFI

