NTSA YAZINDUA TEKNOLOJIA INAYOTUMIA KAMERA ZA CCTV KUIMARISHA USALAMA BARABARANI

Halmashauri ya uchukuzi na usalama barabarani NTSA kwa ushirikiano na wadau katika sekta ya uchukuzi wamezindua teknolojia inayotumia kamera za CCTV kufuatilia usalama wa madereva barabarani na iwapo wanafuatilia kanuni zilizowekwa.
Wakizungumza mjini Mombasa, NTSA imesema kuwa teknolojia hiyo inalenga madereva wa masafa marefu na kudai kuwa asilimia 85 ya ajali zinazoripotiwa nchini ni kutokana na utepetevu wa madereva.
Kulingana na mkurugenzi wa PIONEER SAFETY ROAD Habel Okema Kifaa hicho kitakuwa kinafuatilia matukio ya madereva kutoka Mombasa Hadi Busia mpakani mwa Kenya na Uganda.
Naye Eva Nyawira ambaye ni Meneja wa NTSA kanda ya pwani amesema takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watu elfu nne wamepoteza Maisha kutokana na ajali