WITO WA KUWEPO KWA MABARAZA YA SOKA WATOLEWA

Wito umetolewa kwa viongozi wa michezo katika kaunti za pwani kuungana na kushinikiza wanasiasa waliochaguliwa ili kutimiza ahadi zao.

Ferdinand Mwambire ambaye ni mkufunzi wa soka katika kaunti ya kilifi anasema ni wakati sasa viongozi wa soka katika mkoa mzima wa pwani kuja pamoja na kuanzisha mikakati ya kushinikiza viongozi walioko mahakamani kutimiza ahadi nyingi za michezo walizotoa kwa wananchi kipindi cha kampeni za uchagunzi mkuu uliopita.

Amesema kwamba viongozi wengi wanatelekeza wapiga kura kwa kutotimiza matakwa yao ambayo yanafaa kutumika kuimarisha michezo, na badala yake wanafanya mambo yao binafsi.