WADAU WA SOKA LA MALINDI WALALAMA MAREFA HAWASHIRIKISHWI

Wadau wa soka la kaunti ya Kilifi wanalalama kuhusu kutohusishwa kwa marefa wa kaunti hii katika mechi za daraja la pili kitaifa kwenye mechi zinazochezwa katika kaunti ya Kilifi tofauti na zile zinazochezwa katika kaunti nyingine.

Akizungumza na tama la spoti jioni ya leo mkufunzi Nero Chishenga anasema kwamba uongozi wa soka la daraja la pili unakosa kutumia waamuzi wa kaunti ya Kilifi katika mechi jambo ambalo linaibua maswali mengi ambayo ni pamoja na maonevu kwa vilabu vya kaunti hii.

Chishenga anasema jambo hilo linawafanya kukosa kujivunia waamuzi wao katika harakati za kukuza soka la mashinani licha ya kwamba wapo marefa ambao wana tajiriba ya kuchezesha mechi kubwa.

Ni kauli iliyongunwa mkono na mkufunzi elly katana mkufunzi wa klabu ya malindi progressive academy ambaye amesema kwamba mambo mambo kama hayo yanachangia maonevu katika mechi hatua inalemaza makuzi ya mchezo huo.

Mkufunzi Katana anasema kumekuwa kukishuhudiwa maonevu katika viwanja hasa katika mechi nyingi za ugenini.