WENYE JIJI LA MANCHESTER WAVUNA WIKENDI

Klabu ya Manchester City jana ilisajili ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya klabu ya Aston Villa katika uwanja wao wa nyumbani Etihad. Mabao ya ushindi huo kwa vijana wa Pep Guardiola zyalifungwa na Rodri, goli la ikay Gondogan  katika dakika ya 39 na hatimaye ryad Mahrez kugongelea msumari ushindi huo kupita mkwaju wa penalty kabla kutamatika kwa kipindi cha kwanza.

Kwa upande mwengine Aston Villa walipata bao la kufutia machozi kupitia fowadi Ollie Watkings katika dakika ya 61 ya mchezo.

Manchester United nao wakiwa katika dimba la ugenini Elland Road walisajili ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Leeds United. Bao la Marcus Rashford katika dakika ya 80 lakini pia lile ya Alehandro Garnacho katika dakika ya 85 ndiyo yalotosha kuwapa ushindi vijana hao wa mkufunzi Erik Ten Hag.

Matokeo hayo yanaifanya Manchester United kupanda hadi nafasi ya tatu na alama 46 huku Leed United ikishuka hadi nafasi ya 17.