MUSA OTIENO ASHAURI UTAWALA

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars mwite Musa Otieno ametoa wito kwa viongozi serikalini kuboresha michezo mashinani na kugeuza michezo kuwa ajira kwa vijana mbali na burudani pekee.

Otieno ambaye pia alikuwa mkufunzi wa timu ya taifa ya Kenya anasema serikali inajukumu la kuweka mikakati ya kuvutia wadhamini watakao saidia kujenga sekta hiyo ili kuimarika zaidi.

Haya yanajiri kipindi ambacho Harambee stars inalenga kucheza mechi ya kwanza ya kimataifa baada ya marufuku ya fifa, na Kenya itakuwa inacheza dhidi ya Burundi mwezi machi katika mechi ya kirafiki tarehe 23 na tarehe 28.