WAZAZI MJINI MALINDI KAUNTI YA KILIFI WATAKIWA WALINDA WATOTO WAO

Wazazi wametakiwa kuwalinda watoto wao dhidi ya kujihusisha na mambo maovu wanapokuwa kwenye likizo ndefu ya mwezi wa Disemba.
Haya ni kulingana na chifu wa eneo la Malindi kaunti ya Kilifi, Nicodemus Mwayele ambaye amesema watoto wengi, hutumika katika shughuli za ulanguzi wa mihadarati hasa msimu huu wanapokuwa majumbani.
Amesema kila mzazi anapaswa kuhakikisha anafahamu sehemu ambazo watoto wao watakuwa wakizuru ili kuwadhibiti dhidi ya kutumika visivyo kwenye mambo ambayo huenda yakahatarisha maisha yao.
Aidha, amependekeza wazazi kuwatafutia watoto wao walimu watakaowasaidia kuendeleza masomo ya ziada wakiwa nyumbani badala ya kurandaranda mitaani ovyo.