Mkurugenzi wa utalii na utamaduni kaunti ya Lamu Ali Ahmed amesema wanapania kuimarisha mbuga za wanyamapori ambazo ziko kwenye kaunti ya Lamu pamoja na utalii wa viumbe wa baharini ili kuwavutia watalii zaidi.
Kulingana na Ali utalii wa mbuga bado haujashughulikiwa kikamilifi kama inavyofanyika katika mbuga a Tsavo iliyoko katika kaunti ya Taita Taveta licha ya kaunti ya Lamu kuwa na wanyamapori wengi.
Ali amesema iwapo mbuga zitaimarishwa uchumi wa kaunti ya Lamu utaboreka kwa kiwango kikubwa.
MBUGA ZA WANYAMAPORI KAUNTI YA LAMU KUIMARISHWA

