WAZIRI WA UTALII NCHINI PENINA MALONZA AMEAHIDI KUIMARISHA SEKTA KIVUTIO CHA UTALII CHA FORT – JESUS

Waziri wa utalii nchini Penina Malonza ameahidi serikali kuu itahakikisha inaimarisha kivutio cha watalii cha Fort – Jesus sambamba na maeneo mengine ya kitalii yaliyoko kaunti ya Mombasa.
Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari baada ya kufanya ziara kwenye vituo mbalimbali vya kitalii kaunti ya Mombasa, Malonza amesema hatua hiyo itasaidia kuwavutia watalii zaidi katika taifa hili la Kenya.
Amesema atashirikiana na viongozi wa kaunti hiyo pamoja na wadau mbalimbali ili kufanikisha hilo.
Aidha, kulingana na Malonza atashirikiana pia ipasavyo na wasimamizi wa bustani ya Mama Ngina Water Front ili kuhakikisha eneo hilo linaimarishwa kiusalama.
Kauli yake imeungwa mkono na kamishna wa kaunti ya Mombasa John Otieno ambaye ameahidi kushirikiana na Malonza ili wenyeji waendelee kuzuru maeneo hayo ya kitalii bila kuhofia usalama wao.