Naibu kamishna wa eneo bunge la Msambweni kaunti ya Kwale Kipkoech Lotiatia amewataka wazazi eneo hilo kuwalinda watoto wao msimu huu wa likizo ndefu ya mwezi wa Disemba.
Lotiatia amesema ni vyema kwa wazazi kuwa karibu na watoto wao ili kuwalinda dhidi ya kushawishika kutumia dawa za kulevya na mambo mengine maovu ambayo huenda yakawaathiri na kushindwa kurejea shuleni mwaka ujao wa 2023.
Akizungumza katika eneo la Msambweni Lotiatia amesema visa vya utumizi wa dawa za kulevya umeongezeka kwa asilimia kubwa kutokana na kile ambacho amesema kuchangiwa na wageni wanaozuru eneo hilo la Kitalii.
Kwa upande wake mbunge wa Msambweni Feisal Bader amesema idadi ya vijana walioathirika na utumizi wa mihadarati imeongezeka kwa kiwango kikubwa na kuwaonya vijana katika eneo hilo dhidi ya kutumia dawa za kulevya kwa kisingizio cha ukosefu wa ajira.
WAZAZI ENEO LA MSAMBWENI WAENDELELEA KUHIMIZWA KUWA KARIBU NA WATOTO WAO

