Gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Maitha Mung’aro amesema anapania kuzuru kila eneo bunge kaunti ya Kilifi kama njia moja ya kuwahudumia wenyeji kwa urahisi.
Amesema mpangao huo utaanza kutekelezwa kuanzia mwaka ujao wa 2023 ili kuwapunguzia wenyeji wa kaunti ya Kilifi gharama ya kuzuru kwenye afisi yake kila wanapotaka huduma mbalimbali.
Mung’aro pia ameahidi kutekeleza ujenzi wa makao makuu ya kaunti ndogo ya Kauma eneo bunge la Ganze kaunti ya Kilifi.
GAVANA MUNG’ARO APANIA KUZURU KILA ENEO BUNGE KAUNTI YA KILIFI

