WAWANIAJI TISA WA FKF WAKUBALIWA KUWANIA URAIS

Wagombea wote 9 katika uchaguzi mkuu ujao wa Fkf wameidbinishwa na kamati ya uchaguzi kuendeleza kampeni baada ya ukaguzi wa stakabadhi zao.

Wawaniaji hao walisalimisha stakabadhi zao kandanda house Jumatatu wiki jana na kamati ya uchaguzi imethibitisha kuwa wamepita vigezo vyote vya kupigania urais wa Fkf.

Wagombea hao tisa ambao ni pamoja na Hussein Mohamed ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa Extreme Sports, Naibu rais wa sasa wa Fkf Doris Petra, katibu mkuu wa Gor Mahia Sam Ochola, mchezaji wa zamani Sammy Owino, aliyekuwa rais wa Fkf Sam Nyamweya, Barry Otieno, Tom Alila, Cleophhas Shimanyula pamoja na Chris Amimo wanaanza rasmi kampeni zao kuwinda kura 92 za wawakilishi katika uchaguzi huo wa Kitaifa.

Uchaguzi wa urais utafanyika tarehe 9 mwezi Disemba uku ule wa matawi ya Fkf katika kaunti mbalimbali ukitarajiwa kufanyika mwezi Novemba.

Hata hivyo kuliibuka maswali kuhusu wagombea ambao wamebadilisha nafasi au cheo kuelekea uchaguzi ujao kwa Mfano Nick Mwendwa ambaye ni rais anayeondoka kuwa naibu wa mgombea kama anavyowania na Doris Petra, msajili wa michezo Rose Wasike anasema hilo sio tatizo kwani kwa wanazingatia sheria za fkf kama zilivyo kwa sasa.

Mwendwa na Doris Petra washahudumu kwa miaka nane tayari katika soka la Kenya.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *