Klabu ya Lionel Messi Inter Miami inayoshiriki ligi ya Marekani MLS itakuwa kati ya washiriki wa mashindano ya Kombe la Dunia ngazi ya klabu mwaka 2025.
Hii ni baada thibitisho kutoka kwa rais wa soka Duniani Gianni Infantino.
Mashindano hayo ambayo sasa yatajumuisha timu 32 yatafanyika Marekani mwaka I kuanzia mwezi Juni 15 hadi 3 Julai.
Timu nane kutoka Ulaya, Sita kutoka Marekani kusini, 12 kutoka Bara Asia, Afrika na Marekani Kaskazini wakiwa na vilabu viwili na moja kutoka Marekani ambao ni wwwndaaji wa mashindano hayo na Inter Miami ndio watakaopeperusha bendera hiyo.
Inter Miami walipewa nafasi hiyo baada ya kuonyesha soka bora baada ya kushinda Supporters Cup siku chache zilizopita.

