ENZO MARESCA NA COLE PALMER WASHINDA TUZO ZA SEPTEMBA

Kocha wa klabu ya Chelsea Enzo Maresca ndiye kocha bora wa mwezi September baada ya tuzo hizo kutangazwa rasmi hii leo.

Maresca ameshinda tuzo hiyo ambayo ndiyo yake ya kwanza katika ligi kuu nchini uingereza baada ya kutopoteza mechi hata moja ndani ya mwezi huo.

Chelsea imeshinda mechi tatu na kutoa sare moja.

Kocha huyo mtaliano amehusika kwenye kumfanya pia mchezaji wake Cole Palmer kushinda tuzo la mchezaji bora mwezi huo wa September.

Mwezi September Palmer amefunga mabao matano ya ligi kuu na kutoa assist moja ya bao katika mechi nne pekee alizoshiriki.