WANARIADHA WAPEWE PASIPOTI ZA KIDIPLOMASIA – ABABU

Waziri wa michezo Ababu Namwaba anasema sasa analenga kuanzisha mzungumzo katika wizara hiyo, mazungumzo yanayopania kuwapa wanariadha wa hapa nchini pasipoti za kidiplomasia, wanariadha wawe na uhuru wa kusafiki katika mataifa ya kigeni kuiuza kenya katika suala zima la michezo.
Amesema hadi sasa taifa la kenya linatambulika sana ulaya kutokana ubora wake kwenye riadha hivyo wanariadha wa kenya sasa wanafaa kupewa heshima hiyo ya kipekee.

Hata hivyo kwa sasa suala la matumizi ya dawa za kusisimua misuli ni jambo ambalo linatajwa kuharibia jina taifa la kenya na kama mkakati wa kwanza wa kukabili hilo, Ababu analenga kuanzisha mjadala wa kuweka sheria kali zitakazozuia au hata kuounguza visa hivi vya wanariadha kuripotiwa kutumia dawa za kusisimua misuli , dawa ambazo ni marufuku kutumika kimataifa.

Ababu kwa sasa bado anaendelea na mikutano na wakuu wa vilabu 18 ya ligi kuu pamoja na wakuu wa Kpl kujadili mstakabali wa soka la hapa nchini.
Kufikia sasa Kenya inasalia kufungiwa na fifa kutoshiriki michezo ya soka la kimatafa.