Baadhi ya walimu kaunti ya Taita Taveta wameitaka serikali kuutupilia mbali mtaala mpya wa umilisi wa CBC na badala yake irejeshe ule wa zamani wa 8-4-4.
Wakiongozwa na Paul Maundu walimu hao wamesema mtaala huo una gharama kubwa kwa mzazi huku pia akisema haukishirikisha wadau wote wa elimu kabla ya kuanzishwa kwake.
Maundu amesema uhaba wa walimu utakuwa kizingiti kikubwa cha kuhakikisha mtaala huo unatelekezwa jambo linalosababisha shinikizo zao za kutaka uondolewe.
Kwa upande wao baadhi ya wazazi wakiongozwa na Mercy Mwakisha wamesema itakuwa vyema iwapo CBC itaondolewa kwani tayari gharama ya maisha imepanda na itakuwa mzigo kwa wazazi kugharamia mtaala huo.
BAADHI YA WALIMU TAITA TAVETA WATAKA CBC KUTUPILIWA MBALI

