Baadhi ya wanaharakati wa kimaendeleo katika shirika la kijamii la Kilifi Citizen Forum katika eneo bunge la Kaloleni kaunti ya Kilifi, wamepongeza hatua ya mahakama kubatilisha uamuzi wa serikali kuu, kuagiza mbegu za vyakula vya kisaki yaani GMO.
Kwa mujibu wa wanaharakati hao serikali ya Kenya Kwanza, ilikiuka katiba kwani ili kosa kuwahusisha wananchi, katika utekelezwaji wa suala hilo kwa kuwapatia nafasi ya kutoa maoni yao, kuhusiana na suala hilo kama wanavyofanya kabla ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika jamii.
Wakiongozwa na Sidi Kahati, Said Mumba pamoja na Mercyline Mwavita, wameikosoa vikali serikali ya Kenya kwanza, kwa kile walichosema chakula hicho kilipaswa kuwafaidi wananchi wote, kutokana na ongezeko la bei ya vyakula na hivyo basi ni sharti washirikishwe katika uamuzi huo.
Kauli hizo zimeungwa mkono na Zeinab Kistilo huku Daniel Yaa akidai kuwa uagizaji wa chakula cha Kisaki, ni njia mojawapo ya kuwakandamiza wakulima wa mahindi katika baadhi ya maeneo ya taifa hili.
WANAHARAKATI WA KIMAENDELEO KAUNTI YA KILIFI WAIPONGEZA MAHAKAMA

