Serikali ya kaunti ya Mombasa inapanga kuanzisha mradi wa kazi mtaani kwa vijana msimu huu wa likizo ya disemba mradi ambao ulikuwa ukifanywa na serikali kuu.
Ni mswada ambao ulipendekezwa na kupitishwa bungeni na wawakilishi wa wadi katika bunge la kaunti ya Mombasa juma lililopita.
Akizungumza kwenye kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amepongeza mswada huo akisema utasaidia pakubwa katika kukabili suala la uhalifu miongoni mwa vijana kaunti ya mombasa.
Kulingana naye vijana wataingizwa katika kazi mbalimbali za mikono ili waweze kupata mapato yao ya siku.
Aidha, Nassir amewahakishia usalama wageni wote wanaozuru mjini Mombasa msimu huu wa likizo na sherehe za disemba akisema mombasa iko tayari kupokea wageni.
SERIKALI YA MOMBASA KUANZISHA MRADI WA KAZI MTAANI

