MAAFISA TAWALA ENEO LA VOI WATATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WAZAZI PAMOJA NA MAAFISA WA USALAMA

Maafisa tawala kaunti ndogo ya Voi, kaunti ya Taita Taveta wamesisitiza haja ya ushirikiano baina ya wazazi na asasi za usalama kwa minajili ya kukabiliana na utumizi wa mihadarati katika eneo hilo.
Wakiongozwa na Delphine Mwazo maafisa hao tawala wamesema vijana wengi wanaendelea kuangamia kupitia utumizi wa dawa kulevya huku ongezeko la utumizi ya mihadarati likishuhudiwa zaidi wakati wa likizo ya mwezi wa Disemba.
Mwazo amesema licha ya hamasa za mara kwa mara kuhusiana na athari za utumizi wa mihadarati bado kuna vijana wanaoishia kuwa waraibu wa dawa za kulevya.
Aidha Mwazo amesema kuwa tayari wameweka mikakati ya kushirikiana na wazee wa nyumba kumi sawia na wazee wa mitaa kwa minajili ya kuimarisha hamasa dhidi ya utumizi wa mihadarati.