Hamasa zimezidi kutolewa kwa jamii hasa kwa watoto katika kaunti ya Tana River kuhusu mbinu za kupiga ripoti wakati wanapodhulumiwa kama vile kingono.
Mwendesha mashtaka katika mahakama ya Garsen kaunti ndogo ya Tana Delta Kaunti ya Tana River Ben Kandie ameongoza zoezi la kutoa hamasa hizo kwa makundi ya watoto eneo hilo.
Kandie amewashinikiza watoto kutonyamaza wanapotendewa dhuluma za kingono na badala yake wapige ripoti mara moja kwa wazazi, walimu au hata maafisa tawala.
Wakati huohuo, Juma Kambi ambaye ni mkereketwa wa haki za watoto, amesema ni wakati sasa wa wakaazi kuelewa kwa kina kuhusiana na haki za watoto sawia na sheria zinazowalinda watoto.
Kambi amewataka watoto katika kaunti hiyo kuendekeza maadili miongoni mwa wanajamii wengine sambamba na kuzingatia elimu ili kufaulu katika maisha yao ya siku za usoni.
HAMASA ZAZIDI KUTOLEWA KUHUSU NAMNA YA KUWALINDA WATOTO DHIDI YA KUDHULUMIWA TANA RIVER

