Mkufunzi mkuu wa kikosi cha mpira wa wavu kinachowakilisha kaunti ya kilifi Henry Nyamu ameeleza kuridhishwa kwake na matokeo ya jana ya ushindi wa seti 3-0 dhidi ya kaunti ya embu katika mechi yao ya kwanza ya mashindano ya Kenya Youth Inter County Sports yanayoendelea katika kaunti ya Tharaka Nithi.
Amewapongeza malkia hao wa kaunti ya kilifi kwa kuzidi kujituma katika mashandano hayo akisema kwamba licha ya kuwa na wapinzani wakali bado anaimani watazidi kuandikisha matokeo mazuri.
Mkunfunzi Nyamu amesema ako na matumaini ya kuibuka mabingwa wa mashindano hayo ya mpira wa wavu akitaja kwamba wamekuwa wakipokea msaada mkubwa kutoka kwa waziri wa michezo kaunti ya kilifi DKT Ruth Dama Masha pamoja na Afisa mkuu wa talanta na michezo katika kaunti ya kilifi naftali Owino ambao wamekuwa wakiwatembelea katika kambi zao kuwapa motisha.

