Mataifa matatu jirani (Rwanda, Tanzania na Kenya) yanayounda Jumuiya ya Afrika Mashariki yameanza mchakato wa kuomba kuandaa kwa pamoja mashindano ya Kombe la AFCON mwaka 2027.
Taarifa ya kuanza mchakato huo zimesemwa na Waziri wa Michezo wa Kenya Ababu Namwamba ambaye amesema wameshawasilisha maombi rasmi kwa pamoja huku kushindwa kwa taifa la Namibia na Botswana kukiongeza nguvu ya kushinda.
Waziri Ababu anasema kwamba amefurahishwa na kwamba mchakato huo unawaendea vizuri hiyo kuzidi kuleta matumaini makubwa.
Ikumbukwe kwamba kenya iliwahi kufungiwa kwa zaidi ya mwaka mzima kutokana na marufuku ya fifa baada ya serikali ya kenya kuingilia mambo ya ndani ya shirikisho la soka la FKF.

