WAKEREKETWA WA HAKI ZA KIBINADAMU WAMTAKA RAIS RUTO KUPUNGUZA BEI ZA BIDHAA

Wakereketwa wa maswala ya kijamii wamemtaka rais William Samoei Ruto kupunguza bei za bidhaa kwa kushusha ada na kodi zinazotozwa kwa bidhaa na huduma za kimsingi kama kawi, mafuta na vyakula.
Wakereketwa hao kutoka shirika la kutetea haki za kibinadamu la MUHURI, wakiongozwa na Francis Auma ambaye ni afisa wa dharura katika shirika hilo wamekosoa uamuzi wa rais Ruto kuongeza bajeti ya ofisi ya rais kwa shilingi bilioni tano zaidi ilhali wakenya wengi wanahangaika kutokana na gharama ya juu ya maisha na athari za ukame.
Hili limeibuka siku za hivi karibuni baada ya kubainika kuwa afisi ya rais tayari imemaliza shilingi bilioni 8 ilizokuwa imetengewa kwa miezi sita ya kwanza afisini.
Aidha wakereketwa hao wamesema maafisa wa serikali hawana nia ya kuwaimarisha wakenya kiuchumi kutokana na swala kuwa wameweka mbele matakwa yao nao wakenya wakiendelea kuumia.