SUPKEM YAITAKA SERIKALI KUU KUPIGA MARUFUKU MASHIRIKA YANAYOFADHILIWA NA MATAIFA YA NJE

Baraza kuu la waslamu nchini SUPKEM limeitaka serikali kupiga marufuku mashirika yasiokuwa ya kiserikali yanayofadhiliwa na mataifa ya Ulaya kuunga mkono mapenzi ya watu wa jinsia moja.
Wakiongozwa na sheikh Badru Khamis Baraza hilo pia linaitaka serikali kuhakikisha linalinda wananchi dhidi ya kushirikishwa katika mila na tamaduni za mataifa ya Ulaya hasa mila zinazokinzana na maadili ya kiafrika.
Aidh,a naibu mwenyekiti wa kitaifa wa baraza hilo Sheikh Mohdhar Khitamy amesema licha ya mahakama kuruhusu kusajiliwa kwa mashirika hayo, hawatakubali ushoga na usagaji kuenea nchini.
Kwa upande wake sheikh Abuu Hamza amesema ni sharti serikali ipige marufuku mashirika yote yanaounga mkono mapenzi ya jinsia moja kuhudumu nchini na kuitaka wizara ya elimu nchini pia kuchunguza baadhi ya vitabu wakidai kuwa huenda elimu ya ubasha na usagaji ikaenezwa kwa watoto shuleni.