WAGOMBEA WA FKF KILIFI WAORODHESHWA

Shirikisho la soka limechapisha Orodha rasmi ya wawaniaji wa viti mbalimbali vya Fkf katika kaunti ya Kilifi.

Kama ilivyotarajiwa baada ya Tom Lango afisa wa soka la Malindi kujiondoa kwenye kinyanganyiro cha Uenyekiti sasa wanaogombania kiti hicho wamesaliaa kuwa wawili na ni Mohamed Kai na Mwenyekiti wa sasa Dickson Angore ambaye analenga kutetea kiti hicho.

Dickson Angore amemchukua Mwenyekiti wa soka la eneo bunge la Rabai John Barisa kuwa mgombea mwenza huku Mohamed Kai akisimama na William Tsaka.

Tom Odak ambaye amekuwa msimamizi wa klabu ya Msato kwa muda anavombania kiti cha ukatibu dhidi ya Mwenyekiti Japhet Kaingu anayelenga kuhifadhi nafasi hiyo.

Mohamed Suleiman na Juma Makarani wanagombania kiti cha uweka hazina. Janet Munyazi na Elizabeth Santa wamejitosa kwenye kiti cha uwakilishi wa wanawake huku Edward Karima na James Furaha wakigombania uwakilishi wa vijana.

Uchaguzi wa Fkf katika gatuzi la Kilifi sawa na matawi mengine nchini unatarajiwa kufanyika mwezi ujao huku ule wa urais ukifanyika tarehe 9 mwezi Disemba