Kocha wa timu ya taifa ya Junior starlets Mildred Cheche anasema bado anaimani na kikosi chake na kuwa wataandikisha matokeo mazuri hiyo kesho kwenye mechi ya mwisho dhidi ya Mexico
Cheche anasema Jr starlets katika mashindano haya ya Kombe la Dunia kwenye taifa hilo la Dominican Republic wamekutana na timu zenye Upinzani mkubwa jambo ambalo limewakalia ngumu kupata angalau matokeo mazuri.
Vile vile amewashukuru mashabiki wa Kenya kwa kuendelea kufuatilia mechi zao jambo ambalo anasema linawapa motisha.
Kimberly Akinyi ambaye ni beki wa Jr starlets anasema ana matumaini kesho kikosi Chao kitashinda ili kurudi nyumbani angalau na alama tatu

