Wakuu wa vilabu vya mashinani wanasema wanafurahishwa sana na makuzi ya talanta za soka za vijanza wao katika eneo bunge la magharini kaunti ya kilifi.
Akizungumza na Tama la Spoti alasiri ya leo Kennedy Rimba ambaye ni mkufunzi mkuu wa kikosi cha bosuster kilichojisajili kwa ligi ya fkf ya tawi la eneo bunge hilo amasema kwamba amefurahishwa na kuona vijana wake watatu wamepata heshima ya kipekee ya kufanyiwa majaribio na Super Warrriors ya Nakuru kikosi kinachoundwa na majeshi ya kdf katika kaunti ya nakuru.
Wachezaji walopata fursa hiyo ya kipekee kutoka klabu ya bosuster ni Lemmy kahindi, Ahmed Kajitwa pamoja na George Mwangemi wa klabu ya Masuster.
Ikumbukwe kwamba klabu ya Bosuster wiki jana ilimwachilia mchezaji wao Kahindi Ponda kuenda Ruiru Hotsters klabu inayochezea ligi ya daraja la kwanza kitaifa.
Uhaba wa marefa unazidi kulemaza soka la mashinani kwani mashindano yalokuwa yameandaliwa na fkf tawi la magharini wikendi ilopita yalilazimika kupigwa kalenda kwa muda usojulikana. Rimba ambaye anaongoza klabu ya Bosuster ameeleza tama la spoti kwamba mashindano hayo yalilazimika kusitishwa kwa muda kutokana na marefa kuwa wachache kuendesha michuano hiyo.
Ni mashindano yalokuwa yamelenga kuhusisha vilabu 24 kutoka eneo la gongoni vilabu ambayo vilikuwa vimepangwa katika makundi manne.
Mashindano hayo yalifaa kungoa nanga wikendi ilopita hadi mwezi December mwaka huu wa 2022.

