Toni Kroos kiungo wa soka wa timu ya taifa ya ujerumani ambaye anakipiga katika klabu ya real Madrid hapo jana alipigwa kadi nyekundu ya kwanza katika taaluma yake tangia kuanza rasmi kucheza soka la ushindani mwaka 2006.
Kroos alipokea kadi hiyo katika dakika za lala salama kwenye mechi ya laliga wakati real Madrid walikuwa wanavaana na Gerona dimbani Santiago Barnebou ambako mechi hiyo ilitamatika kwa sare ya bao 1-1.
Kwa matokeo ya wikendi hii Real bado inaselelea kileleni mwa laliga kwa alama 32 alama moja mbele ya Barcelona ambao sasa wako na alama 31 .

